| |
Tathmini ya sekta isiyo rasmi ilifanyika kuanzia Novemba 2004 hadi Septemba, 2005. tathmini ililenga kubaini mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukuwabwa sekta isisyo rasmi, jinsi sekta inavyoendeshwa, athari zake katika uchumi, vizuizi vya kitaasisi na kisheria katika kurasimissha biashara na rasilimali, na vivutiao vinavyosababisha walengwa kuendesha shughuli zao kweney sekta isiyo rasmi.
Shughuli zilizofanywa na matokeo yaliyopatikana katika awamu hii ni pamoja na;,
- Kueleza kwa ufasaha na kubaini maeneo ya sekta isiyo rasmi, ukubwa, aina, thamani, uhusiano wake na vyombo vya sheria, namna na mifumo yake ya utendaji na wahusika wakuu
- Kuanishi vikwazo vikuu katika Taasisi vinavyosabaisha vizuizi vya kisheria, kiutendaji na kiuchumi katika ushiriki wa wanyonge kwenye mfumo rasmi wa kiuchumi.
- Kubaini vikwazo visivyo vya kitaasisi vinavyoathiri jitihada za wadau wa sekta isiyo rasmi kurasimisha rasilimali
- Kuandaa mkakati wa ushirikishwaji wa wadau wote na kampeni za uhamasishaji
- Kujenga msingi utaowezesha kuboresha mfumo wa sheria uliopo ili kufanikisha malengo ya MKURABITA
Matokeo ya Utafiti
Matokeo ya tathmini ya sekta isisyo rasmi yaliibua mambo makuu mawili
- Ilibainishwa kuwa mifumo ya sheira inayoongoza umiliki wa rasilimali nauendeshsji wa ibaisahra ni migumu kutumika kwa wafanyabishara wadogo na wamiliki wa rasilimali. Ufuatiliaji na utekelezaji wa sheria hizo ni mgumu na una ghrama kubwa. Kwa ufupi mifumo na sheria zilizopo hazikidhi mahitaji ya watu maskini, zinabagua na hazina msaada katika kujnga jamii yenye mshikamano. Kutokana na vikwazo hivi, wanajamii wengi hawatumii mifumo hii ya kisheria katika kuendesha shughuli za kiuchumi
- Utafiti ulibaini kuwa Watanzania wengi walio katika sekta isiyo rasmi wamebuni mifumo na taratibu zinazowezesha kupata na kumiliki mali, kuanzisha na kuendesha biashara na kuweka kumbukumbu nje ya mfumo rasmi kama njia ya kuepuka na pingamizi na bugudha za mfumo rasmi na kumiliki rasilimali na kuendesha
Matokeo mahsusi ya utafiti yalionyesha kuwa;
- Asilimia 90 ya Watanzania wanaendesha maisha yao na kupatia kipato chao kupitia sekta isiyo rasmi.
- Sekta isiyo rasmi nchini Tanzania ni kubwa sana, ambapo asilimia 89 ya rasilimali zinamilikiwa nje ya mfumo rasmi
- Kiasi cha asilimi 86 ya rasilimali zilizo mjini(ikiwemo Ardhi) yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 9.4 ziko kwenye sekta isiyo rasmi
- Kati ya hizo, Asilimia 26 ya Ardhi inayomilikiwa kwenye mfumo usio rasmi ipo mkoani Dar es Salaam, na kati ya hiyo, Asilimia 11 ipo kwenye maeneo yaliyopimwa na asilimia zilizobaki zipo katika maeneo ambayo hayajapimwa.
- Gharama za kufidia rasilimali na biashara za sekta isizo rasmi mijini ni takribani billion 11.6 za Kimarekani (sawa na mtaji uliojificha)
- Tahamani ya mmali zote (Mtaji mfu) uliofungiwa katika sekta isisyo rasmi inakadiriwa kuwa Dola za Kimarekani billioni 29.3.
|
|
|
| |
- Hakikisha kuwa mipaka ya kijiji imehakikiwa na kupimwa ipasavyo ili kuepusha migogoro ya mipaka na vijiji jirani
- Kijiji kiwe kimesajiliwa na kupata Cheti cha Ardhi ya Kijiji
- Kijiji kiwe na jengo linalofaa kwa Masjala ya ardhi ya Kijiji
- Maombi ya kupimiwa na kupata hati miliki ya kimila yapelekwe kwenye Halmashauri ya Kijiji kwa ajili ya mapendekezo ya kuidhinishwa
- Maombi lazima yapitishwe na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji
|
|
|
| |
- Kutambuliwa na kuainishwa kwa eneo la urasimishaji na Halmashauri husika katika mji, Manispaa au Jiji,
- Uhamasishaji kwa Uongozi na wananchi wa eneo la urasimishaji,
- Utayarishaji wa michoro ya mipango miji na kuidhinishwa na mamlaka husika,
- Upimaji ardhi ya wananchi kulingana na michoro ya mipango miji
- Uidhinishaji wa ramani za upimaji kwenye mamlaka husika,
- Utayarishaji na utoaji wa Hati za kumiliki ardhi kwa wamiliki wa ardhi iliyopimwa.
|
|
|
|