Semina ya siku mbili ya uhamasishaji kwa viongozi wakuu wa serikali na mashirika mbalimbali juu ya Haki Miliki ilifanyika katika ukumbi wa Karimjee, mnamo Septemba 8 – 9, 2003.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, ndieye aliyekuwa Mwenyekiti wa semina hii kwa siku ya kwanza. Naye aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mheshimiwa Cleopa Davidi Msuya alishika uenyekiti wa semina hii katika siku ya pili.
Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria walikuwa ni mawaziri na manaibu mawaziri wote, wakuu wa mikoa, makatibu wakuu, maafisa wandamizi wa serikali, wakuu wa taasisi za umma, mashirika ya kijamii pamoja na waandishi wa habari.
Aidha semina iliandaliwa lengo ikiwa ni kuwahamasisha na kutoa ufahamu kwa Uongozi wa Tanzania juu ya uwiano uliopo kati ya haki miliki ya rasilimali zilizo rasmi na kukua kwa mitaji na kuengeza pato katika muktadha wa usawa na maendeleo ya kiuchumi yanayojumuisha wengi.
Dr. Hernando de Soto, Rais wa Taasisi ijulikanayo kama ‘Institute for Liberty and Democracy (ILD)’ toka nchini Peru, aliwasilisha juu uzoefu wa muundo wa taasisi hiyo katika urasimishaji wa rasilimali na biashara katika kuunda mfumo mmoja unaowaunganisha haki miliki za rasilimali na biashara.
Bw. John Schjelderup Olaisen, Mkurugenzi Mtendaji wa Norway Registers Development naye aliwasilisha ripoti ya Warsha ya Urasimishaji wa Rasilimali Tanzania iliyofanyika Mei 2003.
Katika semina hii Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa, alitoa hutuba ya ufunguzi ambayo iliwasisismua wengi kwa kusisitiza umuhimu na manfufaa ya urasimishaji wa rasilimali na biashara katika kuwawezesha Watanzania walio wengi kiuchumi na kupunguza umasikini. Dhana hii pia imeainishwa vizuri katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 1995 na 2000.
Katika siku mbili za majadiliano, uongozi wa kitaifa ulitoa azimio la kuanzishwa kwa mpango wa kurasimisha rasilim ali na biashara zisizo rasmi kwa lengo na madhumuni ya kuwawezesha wamiliki wa mali hizi kushiriki katika uchumi rasmi unaosimamiwa na utawala wa sheria. Hii ni pamoja na kuzitumia mali zao zilizokwisha rasimishwa kama dhamana katika kupata mikopo na fursa zinginezo zilizoko katika uchumi wa soko.
Pia Uongozi uliamua kutumia muundo wa ILD wenye awamu nne za utekelezaji ili kupata huduma ya ushauri kutoka katika taasisi hii katika awamu mbili za awali. Yaani awamu ya kwanza na ya pili
Utekelezaji wa awamu mbili za mwanzo ulianza Novemba, 2004 na ulipangwa uwe umekamilika katika kipindi cha miezi 31 na baadaye (Julai 2007). Kutokana na mabadiliko kadhaa utaratibu wa utekelezaii wa awamu hizi mbili (tathmini ya sekta isiyo Rasmi na Uandaajiwa Maboresho) Ulikamilika Julai 2008.
Matokeo ya utekelezaji wa awamu hizi mbili yanapatikana katika:
1. Report on the Diagnosis – provided in the following seven volumes:-
- Volume 1 – Executive Summary
- Volume II – The Legal Economy: Its Archetypes and size
- Volume III – The Legal Economy: Its institutions and costs
- Volume IV – Barriers to using Property and Doing Business nationwide
- Volume VA – Step by Step: The People’s experience of Legal Procedures (Real Estate Procedures)
- Volume VB – Step by Step: The People’s experience of Legal Procedure (Business procedures).
- Volume VI – Supporting Documents
2. Institutional and Legal Reform Proposals provided in seven volumes as follows:-
- Volume I – Executive Summary
- Volume II – Property Formalization – Reform Outlines and Packages for Tanzania Mainland.
- Volume III – Property Formalization Reform Outlines and Packages for Zanzibar
- Volume IV – Business Formalization Reform Outlines and Packages for Mainland Tanzania.
- Volume V – Business Formalization Outlines and Packages for Zanzibar.
- Volume VI – Institutional Arrangements
- Volume VII – Work Plan, Monitoring and Evaluation Framework and Cost Benefit Analysis.
Utekelzaji wa Awamu ya Tatu unaendelea, ambao umejikita zaidi katika utekelezaji wa sheria na mapendekezo mbalimbali ya kitaasisisi yaliyoandaliwa katika Awamu ya Pili ili kusukuma mbele mchakato wa urasimishsaji wa rasilimali na biashara katika sekta isiyo rasmi. Pamoja na Mpango wa utekelezaji wa miaka kumi
Awamu ya Nne kwa kiasi kikubwa inakwenda sambamba na utekelezaji wa Awamu ya Tatu katika kuzinganisha na mitaji rasilimali na biashara zilizorasimishwa na fursa nyinginezo za kiuchumi. Aidha Awamu ya Nne hii zitajumuisha mchakato mzima wa kuweka na kutekeleza mapendekezo yatakayoziunganisha rasilimali zilizorasimishwa na masoko rasmi katika ngazi ya taifa na kimataifa ili kuwezesha mali zilizorasimishwa ktumika kwa Dhamana kwa lengo la kuongeza mitaji na pato.
Kitengo cha Uongozi cha MKURABITA kinaratibu na kusimamia ujengaji uwezo kwa Serikali za Mitaa kwa kuwezesah upatikanaji wa rasilimali zinazohitajika katika kufikia malengo na matokeo yanayotarajiwa, kusimamia na maendeleo ya utekelezaji na ushauri wa kitaalam.
Serikali za Mitaa amabo ndi watekelezaji wakuu wa shughuli za urasimishaji na Wizara mama zitahusika zaidi na uboreshaji wa sheia na mabadiliko ya kitaasisi yenye lengo la kuanzisha kwa mfumo mmoja wa kitaifa wenyekusimamia haki miliki za rasilimali na biashara.
Mapendekezo ya Maboresho na shughuli za utekelezaji ni shughuli ya kudumu itakayowezesha kuwepo kwa mabadiliko kadri itakavyokuwa inatekelezwa kulingana na mahitaji na matakwa ya walengwa wa Mpango huu.
|