| |
|
|
|
|
|
|
| |
| |
Watanzania wengi bado ni maskini na wanakabiliana na mazingira magumu ya kisheria. Mali na biashara zao ziko ndani ya mifumo ya kijamii ambayo si rasmi, ambapo haki nazo haziko katika mfumo wa kisheria wa kumiliki au kuandikishwa rasmi. Wanakosa fursa ya kupata mitaji hata katika jitihada zao za kujiwezesha na kujiendeleza kiuchumi, hawawezi kufanya shughili kwa uwezo wote walio nao.
MKURABITA inalenga kuyaondoa mapungufu haya na kujenga mfumo wa umilikaji wa mali na mitaji ambao unakidhi mahitaji ya wanyonge.
|
|
|
| |
- Hakikisha kuwa mipaka ya kijiji imehakikiwa na kupimwa ipasavyo ili kuepusha migogoro ya mipaka na vijiji jirani
- Kijiji kiwe kimesajiliwa na kupata Cheti cha Ardhi ya Kijiji
- Kijiji kiwe na jengo linalofaa kwa Masjala ya ardhi ya Kijiji
- Maombi ya kupimiwa na kupata hati miliki ya kimila yapelekwe kwenye Halmashauri ya Kijiji kwa ajili ya mapendekezo ya kuidhinishwa
- Maombi lazima yapitishwe na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji
|
|
|
|
|