Utangulizi

MKURABITA ni Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania. Ni Mpango ulioanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpango huu unasimamiwa na Ofisi ya Rais – Ikulu.

Chimbuko la Mpango huu ni mwelekeo wa Sera za Chama cha Mapinduzi (CCM) miaka ya tisini katika kumilikisha uchumi kwa Watanzania ili kuwawezesha kutumia mtaji uliofichika katika rasilimali na biashara zao na hatimaye waweze kushiriki katika mchakato wa uchumi rasmi unaotawaliwa na sheria.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Watanzania Walio wengi wanamiliki rasilimali na kuendesha ambazo hazina uhai wa kisheria katika sekta isiyo rasmi. Mtaji uliofichika katika rasilimali na biashara hizo hautambuliki. Hivyo wamiliki wake hawajumuiki kikamilifu katika uchumi rasmi. Hivyo hawanufaiki na fursa zilizopo pia hawachangii kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.

Kwa hiyo urasimishaji wa rasilimali na biashara unakusudiwa kuzipa rasilimali na biashara za Watanzania walio wengi uhai wa kisheria ambao utawezesha kuwa na sifa tatu muhimu kama zifuatazo zinazowawezesha kukuza mitaji na kuongeza pato:

  • Taratibu za kisheria na kiuchumi zinazoongeza tija, zinazowezesha kusajili aina mbalimbali za biashara, kutenganisha mali binafsi na mali za biashara pamoja na kuongeza ufanisi wa wafanyakazi.
  • Uwezo wa kisheria wa kufanya biashara katika soko pana lenye mtandao mpana zaidi ya ndugu, jamaa na majirani.
  • Mfumo rasmi wa umiliki mali ambao huipa mali utambulisho maalum na kuipa mali uwezo wa kuhamishika katika soko pana kulingana na fursa zilizopo pamoja na kuongeza thamani ya mali.

MKURABITA ni sehemu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) na Mkakati wa Kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA), ukilenga kuwawezesha walengwa kutumia rasilimali na biashara zao zilizo rasimishwa katika kujipatia mitaji, soko pana na fursa zingine zinazopatikana katika sekta rasmi na hivyo kupunguza umaskini wa kipato.


 
 
  • Hakikisha kuwa mipaka ya kijiji imehakikiwa na kupimwa ipasavyo ili kuepusha migogoro ya mipaka na vijiji jirani
  • Kijiji kiwe kimesajiliwa na kupata Cheti cha Ardhi ya Kijiji
  • Kijiji kiwe na jengo linalofaa kwa Masjala ya ardhi ya Kijiji
  • Maombi ya kupimiwa na kupata hati miliki ya kimila yapelekwe kwenye Halmashauri ya Kijiji kwa ajili ya mapendekezo ya kuidhinishwa
  • Maombi lazima yapitishwe na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji
 
 
  • Kutambuliwa na kuainishwa kwa eneo la urasimishaji na Halmashauri husika katika mji, Manispaa au Jiji,
  • Uhamasishaji kwa Uongozi na wananchi wa eneo la urasimishaji,
  • Utayarishaji wa michoro ya mipango miji na kuidhinishwa na mamlaka husika,
  • Upimaji ardhi ya wananchi kulingana na michoro ya mipango miji
  • Uidhinishaji wa ramani za upimaji kwenye mamlaka husika,
  • Utayarishaji na utoaji wa Hati za kumiliki ardhi kwa wamiliki wa ardhi iliyopimwa.
 

   
 
Jumla 17848