Mantiki
Rasilimali na biashara katika sekta isisyo rasmi hazina uhai kisheria mtaji ulifichika katika rasilimali na biashara hizo hautambuliki. Pia wamiliki wake hawajumuiki na kushiriki kikamilifu katika uchumi rasmi. Hivyo hawanufaiki na fursa zilizopo vile vile hawachangii ipasavyo katika kukuza uchumi wa nchi.
Dhana
Dhana ya MKURABITA ni UWEZESHAJI wa wananchi ili waweze kutumia rasilimali na biashara zao kama chanzo cha kujiongezea mitaji na nyenzo ya kupanua wigo wa ushiriki katika soko la ndani na nje ya nchi.
Hakikisha kuwa mipaka ya kijiji imehakikiwa na kupimwa ipasavyo ili kuepusha migogoro ya mipaka na vijiji jirani
Kijiji kiwe kimesajiliwa na kupata Cheti cha Ardhi ya Kijiji
Kijiji kiwe na jengo linalofaa kwa Masjala ya ardhi ya Kijiji
Maombi ya kupimiwa na kupata hati miliki ya kimila yapelekwe kwenye Halmashauri ya Kijiji kwa ajili ya mapendekezo ya kuidhinishwa
Maombi lazima yapitishwe na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji
Kutambuliwa na kuainishwa kwa eneo la urasimishaji na Halmashauri husika katika mji, Manispaa au Jiji,
Uhamasishaji kwa Uongozi na wananchi wa eneo la urasimishaji,
Utayarishaji wa michoro ya mipango miji na kuidhinishwa na mamlaka husika,
Upimaji ardhi ya wananchi kulingana na michoro ya mipango miji
Uidhinishaji wa ramani za upimaji kwenye mamlaka husika,
Utayarishaji na utoaji wa Hati za kumiliki ardhi kwa wamiliki wa ardhi iliyopimwa.