Maswali ya mara kwa mara

MKURABITA ni nini?

Ni kifupi cha maneno "Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania". Ni mpango ulioanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukilenga kuwapa nguvu kiuchumi, wananchi hasa wale wa kipato cha chini (wanyonge) vijijini na mijini, kwa kuwaongezea uwezo wa kumiliki rasilimali na kufanya biashara katika mfumo rasmi wa kisasa, unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni rasmi za kiutawala.


 
 
  • Hakikisha kuwa mipaka ya kijiji imehakikiwa na kupimwa ipasavyo ili kuepusha migogoro ya mipaka na vijiji jirani
  • Kijiji kiwe kimesajiliwa na kupata Cheti cha Ardhi ya Kijiji
  • Kijiji kiwe na jengo linalofaa kwa Masjala ya ardhi ya Kijiji
  • Maombi ya kupimiwa na kupata hati miliki ya kimila yapelekwe kwenye Halmashauri ya Kijiji kwa ajili ya mapendekezo ya kuidhinishwa
  • Maombi lazima yapitishwe na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji