How Do I?
Business Formalization
Katika kurasimisha Biashara mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:
- Sajili jina la biashara BRELA kupitia mtandao, Ofisi ya idara ya Biashara au kupitia Vituo Jumuishi vya Urasimishaji na Uendelezaji Biashara vilivyopo katika baadhi ya Halmashauri.
- Uwe na Mkataba wa pango mahali utakapofanyia biashara.
- Pata Namba ya Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA).
- Pata leseni ya Biashara kutoka Halmashauri yako mahali biashara ilipo.
- Fungua akaunti ya benki kwa ajili ya shughuli zako za biashara.
- Tunza kumbukumbu za mahesabu yako vizuri ili uweze kupima uhai wa biashara yako.
- Kama una wafanyakazi hakikisha wana Mikataba ya Ajira.
- Kata bima kwa ajili ya kuilinda biashara yako na majanga yasiyotarajiwa mfano, moto, wizi, mafuriko na majanga mengineyo.
- Hudhuria Mafunzo ya Urasimishaji na Uendelezaji Biashara yanayotolewa katika Vituo Jumuishi vya Urasimishaji na Uendelezaji Biashara.
- Ongeza Mtaji wa Biashara yako kwa kukopa kutoka Taasisi za Fedha