Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

Organization Structure

ORGANIZATION STRUCTURE

MKURABITA ni Mpango ulioanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao unasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais - Ikulu. Utekelezaji wa MKURABITA unasimamiwa na Kamati ya Uongozi yenye jukumu la kutoa Sera na Miongonzo kwa ajili ya Utekelezaji wa shughuli za Urasimishaji. Shughuli za kila siku za MKURABITA husimamiwa na Kitengo cha Uongozi ambacho huongozwa na Mratibu wa Mpango ambaye ndiye Mtendaji Mkuu na huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mratibu wa Mpango husaidiwa na Timu ya Menejimenti katika kuhakikisha utekelezaji wa MKURABITA unafikia malengo.