Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

About 272 Certificates of Customary Right of Occupancy (CCROs) Were Issued to Occupiers in Mkundi Village in Kilosa District


Jumla ya mashamba 272 ya wakulima wadogo wa miwa katika Kijiji cha Mkundi, Kata ya Dumila, wilayani Kilosa, Morogoro yamerasimishwa kwa lengo la kuyapatia Hati Miliki za Kimila zitakazotumika kama nyenzo ya kuwakwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuzitumia kwa kuweka dhamana katika kukopa fedha benki na taasisi zingine za kifedha ili kuendeleza mashamba yao na shughuli nyingie za kiuchumi.

Zoezi hilo la urasimishaji limewezeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ambapo upimaji mashamba uliongozwa na Meneja wa Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango huo, Bw. Anthony Temu kwa ushirikiano na maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Sambamba na upimaji wa mashamba hayo, pia, wameendesha mafunzo kwa wanakijiji waliorasimisha mashamba yao yanayohusu, kanuni za kilimo bora cha miwa, faida za uanzishwaji wa vyama vya ushirika, utunzaji kumbukumbu za mahesabu, uthaminishaji mali, kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi na faida za kujiunga na huduma za benki. Mafunzo hayo yalishirikisha wataalam kutoka kwenye mabenki ikiwemo CRDB na NMB.