Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

BALOZI NJOOLAY AAGWA, APONGEZWA, AIMWAGIA SIFA MKURABITA KWA UCHAPAKAZI


MWENYEKITI wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), anayemaliza muda wake, Balozi Daniel Ole Njoolay ameishukuru Menejimenti na watumishi wa mpango huo kwa kuwa wasikivu kutekeleza maagizo waliyokuwa wanawapatia ndani ya miaka mitatu ya uongozi wao.