Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

International Women's Day


Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo endelevu..Jitokeze kuhesabiwa

Machi 8 ya kila mwaka ni Siku ya Wanawake Duniani ambayo kwa zaidi ya miaka 100 huadhimishwa kimataifa. Baadhi ya wanahistoria wanaeleza kuwa siku hii ilianza 1908 nchini Marekani ikiwa ni jitiahada za wanawake wapatao 15,000 walioandamana wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Inasemekana mwaka mmpja baadaye Chama cha Kisoshalisti huko Marekani kilitangaza tarehe 8 Machi kuwa ni ya wanawake kitaifa.

Pia inaelezwa kwamba mwaka 1910 mwanaharakati wa Kijerumani Clara Zetkin akiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark alitoa wazo na kupendekeza Machi 8 kuwa siku ya wanawake duniani. Katika kikao hicho wanwake wapatao 100 waliowakilisha nchi 17 kwa pamoja waliridhia wazo hilo. Hivyo mwaka 1911 kwa mara ya kwanza siku ya wanawake duniani katika nchi za Austria, Denmark,Ujerumani na Switzerland.

Tangu wakati huo, inaadhimisha siku hiyo kwa kuangazia masuala yanayowahusu wanawake katika maeno mbalimbali duniani. Kauli Mbiu kwa mwaka 2022ni “..Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu..Jitokeze kuhesabiwa..”.

Watumishi wanawake wa MKURABITA wanaungana na wanawake wengine duniani katika kuadhimisha siku hii.