Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

MENEJA MKURABITA AKAGUA MIZINGA 30 ITAKAYOTOLEWA MSAADA KATIKA KIJIJI CHA LUGODALUTALI MUFINDI


Meneja Urasimishaji Rasilimali Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Anthony Temu amekagua utengenezaji wa mizinga 30 katika karakana ya useremala ya Twaha mjini Mafinga, itakayotolewa na MKURABITA kwa wanufaika wa MKURABITA katika Kijiji cha Lugodalutali wilayani Mufindi Iringa.

Wakati wa Ukaguzi huo, Temu aliambatana na Afisa Nyuki wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Khamis Kapilima anayeelezea kitaalamu kuhusu mizinga hiyo.

Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya MKURABITA, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay kwa moja ya vikundi nufaika wa MKURABITA kwa ajili ya kuendesha mradi wa ufugaji wa nyuki kibiashara kuvuna asali, nta na bidhaa zingine.

Mizinga hiyo inatarajiwa kukabidhiwa kesho Mei Mosi wakati wa mafunzo kwa wanufaika zaidi ya 300 wa MKURABITA wenye hati miliki za kimila katika Kijiji hicho cha Lugodalutali.

Mafunzo hayo yataendeshwa na wataalamu kutoka MKURABITA, maofisa wa benki, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambapo watafundishwa jinsi ya kutumia hatimiliki za kimila kukopa fedha benki kwa kuweka kama dhamana, kanuni bora za kilimo, uthamini wa mali, utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za miradi, kuchangamkia fursa mbalimbali na ufugaji bora wa nyuki.

Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Anthony Temu alikagua utengenezaji wa mizinga 30 katika karakana ya useremala ya Twaha mjini Mafinga, iliyotolewa kwa wanufaika wa MKURABITA katika Kijiji cha Lugodalutali wilayani Mufindi, Iringa.

Wakati wa Ukaguzi huo, Temu (kwenye picha aliyevaa koti jeusi) aliambatana na Afisa Nyuki wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Khamis Kapilima anayeelezea kitaalamu kuhusu mizinga hiyo.

Mizinga hiyo imetolewa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya MKURABITA, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay kwa moja ya vikundi nufaika wa urasimishaji kwa ajili ya kuendesha mradi wa ufugaji wa nyuki kibiashara kuvuna asali, nta na bidhaa zingine.

Mizinga hiyo ilikabidhiwa Jumanne ya tarehe moja Juni 2021 wakati wa mafunzo kwa wanufaika zaidi ya 300 wa Urasimishaji wenye hati miliki za kimila katika Kijiji hicho cha Lugodalutali.

Mafunzo hayo yameendeshwa na wataalam kutoka MKURABITA, maofisa wa benki, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambapo walifundishwa jinsi ya kutumia hatimiliki za kimila kukopa fedha benki kwa kuweka kama dhamana, kanuni bora za kilimo, uthamini wa mali, utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za miradi, kuchangamkia fursa mbalimbali na ufugaji bora wa nyuki.