Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

“..Sasa tumejipanga kwenda kurasimishaj ardhi ya Vijiji vya Makanda na Msisi, Wilayani Bahi.."


Kwa takriban wiki moja Timu ya Usimamizi wa Mipango Shirikishi ya Matumizi ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imeendelea na mafunzo elekezi ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa urasimishaji ardhi katika vijiji vya Msisi na Makanda, Mafunzo hayo yaliyowezeshwa na MKURABITA yana lenga katika kuijengea uwezo Halmashauri ya Wilaya yenye jumla ya vijiji 59 kuweza kuanzisha mchakato wa urasimishaji rasiliomali ardhi katika vijiji hivyo kulingana na sheria ya ardhi ya vijiji namba tanoya mwaka 1999.

Katika kuanzakwa mchakato huo Serikali kupitia MKURABITA itawezesha urasimishaji wa mashamba yapatayo 3,000 katika vijiji hivyo pamoja na ujenzi wa masjala za aerdhi za vijiji hivyo. Katika utekelezaji wa zoezi hilo wajumbe katika ngazi mbalimbali wameweza kuhamasishwa na kupata mafunzo elekezi ikiwa ni sehemu ya kuweka misingi muhimu kwa ajili ya uendelevu wa mchakato huo. Wajumbe walipata fursa ya kupewa elimu na hamasa nipamoja na CMT, Hamashauri ya Kijiji na kamati za uhakiki ikiwa ni pamoja na timu ya usimamizi wa mipango shirikishi ya matumizi ya ardhi .

Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa katika vijiji vya Msisi na Makanda kwa takriban miezi mitatu ikiwani pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa masjala za ardhi. Wananchi katika vijiji hivi wameishukuru serikali kupitia MKURABITA kuwezesha utekelezaji wa shughuli hii ambayo wamekiri kuwa urasimishaji umekuja kwao kuwakomboakiuchumi. Hivyo wameahidi kutoa ushjirikiano wakati wote wa utekelezaji wa kazi hii katika vijiji vya na kuwa mabalozi wazuri wa urasimishaji wa ardhi.

Tanzania Census 2022