Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

UZINDUZI PROGRAMU YA MAFUNZO YA URASIMISHAJI BODABODA NA BAJAJI


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mbunge) amezindua Programu ya Mafunzo kwa wafanyabiashara wa Bodaboda na Bajaji Jijini Dodoma.

Akizindua Programu hiyo, Mhe.Ndejembi ameupongeza Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABIKA) kuanzisha mafunzo ya kurasimisha biashara hizo kwa lengo la kuaminika na Taasisi za Fedha ili waweze kupata mikopo na kuweza kumiliki bodaboda na bajaji.

Mhe. Ndejembi ametoa wito kwa vijana waendesha bodaboda na bajaji kujitokeza kwa wingi wakati wa mafunzo katika kata zao na kuwapa taarifa wenzao kuhusu umuhimu wa maafunzo hayo.

Akimwakilisha Mratibu wa Mpango, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu Kasyenene amemshukuru, Mhe.Ndejembi kuzindua programu hiyo ambayo mafunzo yanatarajiwa kuanza Jumatatu katika Kata 41 za Dodoma Mjini na kushirikisha zaidi ya waendesha bodaboda/ bajaji 2500 wanawake kwa wanaume.